Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa azimio hilo vikwazo hivyo vinatazamiwa kuondolewa ifikapo tarehe 18 mwezi Oktoba. Akizungumzia juhudi zinazofanywa na Marekani katika uwanja huo hapo siku ya Jumanne, Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba juhudi zinazofanywa na Marekani kwa lengo la kurefushwa muda wa silaha dhidi ya Iran hazitakuwa na natija yoyote.
Tokea mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran imekuwa ikiwekewa vikwazo vikali vya silaha ili kuidhoofisha na kuifanya isiweze kujilinda na kujitetea dhidi ya maadui zake. Katika hatua ya kwanza, serikali ya Jimmy Carter iliiwekea Iran vikwazo vya kuuziwa silaha baada ya wanachuo wafuasi wa msimamo wa Imam Khomeini (MA) kuteka pango la ujasusi la Marekani mjini Tehran. Baada ya hapo serikali ya Ronald Reagan alizishinikiza serikali nyingine za dunia kutoiuzia silaha Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi chote cha vita vya kulazimishwa.
Kwa mujibu wa azimio hilo vikwazo hivyo vinatazamiwa kuondolewa ifikapo tarehe 18 mwezi Oktoba. Akizungumzia juhudi zinazofanywa na Marekani katika uwanja huo hapo siku ya Jumanne, Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba juhudi zinazofanywa na Marekani kwa lengo la kurefushwa muda wa silaha dhidi ya Iran hazitakuwa na natija yoyote.
Tokea mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran imekuwa ikiwekewa vikwazo vikali vya silaha ili kuidhoofisha na kuifanya isiweze kujilinda na kujitetea dhidi ya maadui zake. Katika hatua ya kwanza, serikali ya Jimmy Carter iliiwekea Iran vikwazo vya kuuziwa silaha baada ya wanachuo wafuasi wa msimamo wa Imam Khomeini (MA) kuteka pango la ujasusi la Marekani mjini Tehran. Baada ya hapo serikali ya Ronald Reagan alizishinikiza serikali nyingine za dunia kutoiuzia silaha Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi chote cha vita vya kulazimishwa.
Kwa kuanzisha mikataba mipya ya ushirikiano wa kiulinzi, Iran imeingia katika awamu mpya ya stratijia ya usalama na ulinzi wa eneo. Mkataba wa aina hiyo uliotiwa saini hivi karibunbi kati ya Iran na Syria unaonyesha wazi kwamba harakati za Marekani za kujaribu kurefusha muda wa vikwazo vya Iran hazitavuruga kwa vyovyote vile stratejia za muda mrefu za kijeshi na kiulinzi za Iran. Ni wazi kuwa Iran itatumia stratijia hizo wakati wowote itakoona kuwa unafaa katika kulinda maslahi yake ya kitaifa.
Bila shaka serikali ya hivi sasa ya Marekani inataka kujidhihirisha kuwa imechukua hatua kubwa ya kubana nguvu za kijeshi za Iran ili iweze kushinda katika uchaguzi mkuu ujao wa rais. Pamoja na hayo matamshi yaliyotolewa karibuni na Waziri wa Ulinzi wa Iran kuhusu suala hilo ni jibu tosha kwa ndoto hiyo ya Marekani. Amir Hatami amesisitiza kwa kusema: Kurefushwa vikwazo vya Iran ni takwa la kijuba na lisilo la kimantiki na wala nchi za dunia hazitalikubali.
342/